2 Samuel 22:2-32

2 aAkasema:

Bwana ni mwamba wangu,
ngome yangu na mwokozi wangu,
3 bMungu wangu ni mwamba wangu,
ambaye kwake ninakimbilia,
ngao yangu na pembe ya wokovu wangu.
Yeye ni ngome yangu, kimbilio langu
na mwokozi wangu,
huniokoa kutoka kwa watu wenye jeuri.
4 cNinamwita Bwana, anayestahili kusifiwa,
nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu.

5 d“Mawimbi ya mauti yalinizunguka,
mafuriko ya maangamizi yalinilemea.
6 eKamba za kuzimu
Kuzimu kwa Kiebrania ni Sheol, maana yake ni Shimo lisilo na mwisho.
zilinizunguka,
mitego ya mauti ilinikabili.
7 gKatika shida yangu nalimwita Bwana,
nilimlilia Mungu wangu.
Kutoka Hekaluni mwake alisikia sauti yangu,
kilio changu kikafika masikioni mwake.

8 h“Dunia ilitetemeka na kutikisika,
misingi ya mbingu ikatikisika,
vilitetemeka kwa sababu
alikuwa amekasirika.
9 iMoshi ukapanda kutoka puani mwake,
moto uteketezao ukatoka kinywani mwake,
makaa ya moto yawakayo
yakatoka ndani mwake.
10 jAkazipasua mbingu akashuka chini,
mawingu meusi yalikuwa chini ya miguu yake.
11 kAlipanda juu ya kerubi akaruka,
akapaa juu kwa mbawa za upepo.
12 lAlifanya giza hema lake la kujifunika:
mawingu meusi ya mvua ya angani.
13 mKutokana na mwanga wa uwepo wake
mawingu yalisogea,
ikanyesha mvua ya mawe
na umeme wa radi.
14 n Bwana alinguruma kutoka mbinguni,
sauti ya Aliye Juu Sana ilisikika.
15 oAliipiga mishale na kutawanya adui,
umeme wa radi na kuwafukuza.
16 pMabonde ya bahari yalifunuliwa,
na misingi ya dunia ikawa wazi
kwa kukaripia kwake Bwana,
kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwake.

17 q“Alinyoosha mkono kutoka juu na kunishika;
alinitoa kutoka kilindi cha maji makuu.
18 rAliniokoa kutoka adui wangu mwenye nguvu nyingi,
kutoka adui zangu waliokuwa na nguvu nyingi kuliko mimi.
19 sWalinikabili siku ya msiba wangu,
lakini Bwana alikuwa msaada wangu.
20 tAlinileta nje mahali penye nafasi tele,
akaniokoa kwa kuwa alipendezwa nami.

21 uBwana alinitendea sawasawa na uadilifu wangu;
sawasawa na usafi wa mikono yangu amenilipa.
22 vKwa maana nimezishika njia za Bwana;
sijatenda ubaya nikamwacha Mungu wangu.
23 wSheria zake zote zi mbele yangu,
wala sijayaacha maagizo yake.
24 xNimekuwa sina hatia mbele zake,
nami nimejilinda nisitende dhambi.
25 y Bwana amenilipa sawasawa na uadilifu wangu,
sawasawa na usafi wangu machoni pake.

26 z“Kwa yeye aliye mwaminifu unajionyesha kuwa mwaminifu,
kwa asiye na hatia unajionyesha kutokuwa na hatia,
27 aa abkwa aliye mtakatifu unajionyesha kuwa mtakatifu,
lakini kwa aliyepotoka unajionyesha kuwa mkaidi.
28 acWewe huwaokoa wanyenyekevu,
lakini macho yako ni juu ya wenye kiburi
ili uwashushe.
29 adWewe ni taa yangu, Ee Bwana.
Bwana hulifanya giza langu
kuwa mwanga.
30Kwa msaada wako naweza kushinda jeshi,
nikiwa pamoja na Mungu wangu
nitaweza kuruka ukuta.

31 ae“Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu;
neno la Bwana halina dosari.
Yeye ni ngao kwa wote
wanaokimbilia kwake.
32 afKwa maana ni nani aliye Mungu
zaidi ya Bwana?
Ni nani aliye Mwamba
isipokuwa Mungu wetu?
Copyright information for SwhNEN